Disseminating information for economic prosperity.
  • Sign In
  • Sign Up
Logo
  • Home
  • About
  • Sectors
    • Governments
    • Non Government
  • Publications
    • Past Presidents
    • Friends of Tanzania
    • Inspirational Icon
    • Magazine
    • Advertismemt Rate
  • Contact us
    • Contact Page
    • Add Business Card

blog details

Ministry of Finance and Planning

P.O. Box 1154, Vuga Street, Zanzibar

+255 242 2343342​

info@mofzanzibar.go.tz

https://mofzanzibar.go.tz/

  • About
  • Team
  • Gallery
  • News

Utangulizi wa ORFM

Kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 Nyanja zote kuu za kiuchumi zilimilikiwa na Mabepari wa Kikoloni. Wananchi wazalendo wa visiwa vya Zanzibar hawakuwa na hisa wala mgao katika uchumi wa Taifa lao. Mapinduzi haya pamoja na malengo mengine yalilenga kurudisha uchumi chini ya mamlaka ya wananchi ili waweze kunufaika na uchumi wa nchi yao. Hivyo baada tu ya Mapinduzi, Nyanja kuu zote za uchumi zilitaifishwa na kuwa chini ya Serikali hali iliyopelekea kuundwa kwa taasisi zinazohusika na kuratibu masuala ya Fedha, Uchumi na Maendeleo ya Zanzibar kwa ujumla.

Taasisi inayoshughulikia fedha, uchumi na mipango ya maendeleo ni moja kati ya taasisi zilizoanzishwa tokea mwanzoni mwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tokea mwaka 1964 hadi sasa, muundo wa taasisi hizi umekuwa ukibadilika ili kuendana na wakati, mahitaji na matarajio ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Utekelezaji wa shughuli za taasisi hizi umekuwa ukizingatia jinsi majukumu yalivyoainishwa katika hati ya majukumu ya Serikali.

Katika miaka ya 1964 – 1973, taasisi hizi zilikuwa zinafanya kazi kama Ofisi inayoshughulikia fedha chini ya Afisi ya Mwenyekiti wa Afro Shirazi Party (ASP) Kazi zote za Fedha. Vile vile shughuli za Uchumi na Maendeleo ya nchi nazo zilikuwa chini ya Afisi ya Rais Kazi maalum. Mnamo miaka ya 1974, Taasisi iliyokuwa inashughulikia masuala ya Fedha ilikuwa na maeneo mawili makuu ambayo ni Hazina iliyokuwa inashughulikia masuala ya fedha, mapato na matumizi na masuala ya maendeleo yalikuwa chini ya uratibu wa Ofisi Kuu ya Kazi za Maendeleo (OKM). Katika kutekeleza kazi za mipango na maendeleo, chombo maalum cha Tume ya Mipango kiliundwa ili kusimamia maandalizi na utekelezaji wa mipango pamoja na kutoa ushauri.  Mwaka 1975 Tume ya Mipango ilikuwa kama Idara ndani ya Ofisi ya Kazi za Maendeleo hadi mwaka 1978 ilipoundwa upya na kuitwa Tume ya Kudumu ya Mipango (TKM) kama chombo kinachojitegemea.

Kuanzia mwaka 1978, Taasisi za Fedha na Mipango ziliunganishwa na kufanya Wizara moja iliyojulikana kwa jina la Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango.

Kufikia mwaka 1982 taasisi hizi ziligawika na kuundwa wizara mbili tafauti; Wizara ya Fedha na Wizara ya Nchi

Afisi ya Rais Mipango kati ya miaka 1984 na 1987, taasisi hizi ziliendelea kuwa tofauti chini ya Mawaziri na Makatibu tofauti kama inavyoonekana katika Sura ya Tatu.

Katika mwaka 1988, Wizara ya Mipango na Wizara ya Fedha ziliunganishwa tena na kuwa Wizara ya Fedha na Mipango. Wizara hii iliundwa na taasisi tatu kuu za Idara ya Baraza la Mipango (Planning Council); Kamati ya Uchumi ya Baraza la Mapinduzi (Economic Committe of Revolutionary Council); na Tume ya Mipango (Planning Commission) zilizokuwa zinasimamia masuala ya uchumi na mipango ya maendeleo nchini.  Katika miaka iliyoanzia 1988, kulitokea mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi yaliyopelekea Wizara za Serikali kupewa mamlaka ya kusimamia na kuratibu mashirika ya Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Kwa miaka ya 1990 – 2000, utekelezaji wa shughuli za fedha na mipango ziliendelea kuwa tofauti kwa kuwepo Wizara inayoshughulikia Fedha na Ofisi ya Rais, Mipango na Vitega Uchumi iliyokuwa ikushughulikia mipango ya Kitaifa na Uwekezaji Nchini. Muundo wa Wizara kuanzia mwaka 2000-2010 uliziunganisha taasisi hizi mbili na kuwa Wizara ya Fedha na Uchumi ambapo kulikuwepo na Idara kumi na moja na kusimamia taasisi tisa zinazojitegemea.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 uliomuweka madarakani Dr. Ali Mohammed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, Taasisi hii ilibadilishwa jina na kuwa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo yenye Idara kumi na moja na kusimamia Taasisi tisa zinazojitegemea.


DIRA:
Kuwa ni taasisi bora yenye kuhakikisha upatikanaji na matumizi bora ya fedha za Serikali kwa utekelezaji wa mipango yenye kuleta tija kwa maendeleo ya nchi na wananchi.

DHAMIRA:
Kusimamia vyema mipango ya maendeleo ya nchi, kubuni vyanzo vipya vya mapato ya Serikali na kusimamia rasilimali za Serikali kwa kuhakikisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za Serikali.


Hon. Dr. Juma Malik Akil
Minister
Hon. Dr. Hamad Omar Bakari
Deputy Minister
Blog Image

Judge Mark Bomani, The First Indigenous Attorney General

07 - October - 2025
Blog Image

Ambassador Amina Salum Ali, Tanzania’s woman of class

07 - October - 2025
Blog Image

A photographer’s critique of photography

07 - October - 2025

Popular Companies


Service

Mohammed Enterprises Tanzania Limited

GROUP OF COMPANIES
Service

President of Tanzania

GOVERNMENT OF TANZANIA
Service

Ministry of Information, Culture, Arts and Sports

GOVERNMENT OF TANZANIA
Service

Ministry of State President's Office, Labour, Economic Affairs and Investment

GOVERNMENT OF ZANZIBAR
Service

Clouds Media Group

MEDIA & ADVERTISEMENT
Service

Ministry of State, Prime Minister's Office - Regional Administration and Local Government

GOVERNMENT OF TANZANIA

Logo

Who’s is who Tanzania is an annual publication which addresses in detail the solution of accessing information in one location.

Pages

  • Home
  • About Us
  • Contact
  • Inspiration Icon

Contents

  • Industries
  • Magazine
  • Friends of Tanzania
  • Advertismemt Rate

Address

  • Twiga House, Floor No.7, Samora Avenue
  • info@whoiswhotanzania.co.tz
  • +255 652 272 339

whoswhotanzania © 2024 all rights reserved

Magazine Subscription Form


Cross
  • Home
  • About
  • Companies
  • Magazine
  • Advertismemt Rate
  • Past Presidents
  • Friends of Tanzania
  • Inspiration Icon
  • Contact Us